WAKATI WENGINE WAKIMPONDA RADAMEL FALCAO KWA KUCHEZA CHINI YA KIWANGO, KOCHA WA MAN UNITED LOUIS VAN GAAL AMSIFIA NA KUSEMA UPO MKAKATI WA KUMFANYA AWE BALAA UWANJANI!!

MANCHESTER UNITED inafanya mkakati wa kumwezesha Radamel Falcao awe bora zaidi.
Hilo limetamkwa na Meneja wa Manchester United Louis van Gaal hii Leo.
Falcao, Straika wa Colombia mwenye Miaka 29, amefunga Bao 4 katika Mechi 20 tangu atue Man United mwanzoni mwa Msimu kwa Mkopo kutoka AS Monaco.
Akiongea
hii Leo na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Jumapili ya Ligi Kuu
England Uwanjani Old Trafford na Tottenham Hotspur, Van Gaal ameeleza:
"Tunatafuta suluhisho. Unaweza kuwa mzuri Nchi nyingine lakini ulipo
ikawa tofauti! Hii si mara ya kwanza na ya mwisho!" Baada ya kupigwa Benchi Jumatatu iliyopita kwenye Mechi ya FA CUP na Arsenal, Falcao alichezeshwa kwenye Kikosi cha Vijana U-21 dhidi ya Tottenham Siku ya Pili yake.
Meneja
Van Gaal ameeleza hakumpeleka Falcao huko kumdhalilisha ila kumjenga
zaidi baada ya Msimu uliopita kuumia vibaya Goti lake.
Falcao
yuko kwa Mkopo Man United hadi mwishoni mwa Msimu kutoka AS Monaco ya
France kwa makubaliano kuwa Uhamisho huo unaweza kuwa wa kudumu kwa Dau
la Pauni Milioni 43.2.
0 maoni:
Chapisha Maoni