MECHI
za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONS LIGI
zinaanza kuchezwa Jumanne Usiku Machi 10 kwa Mechi mbili. Huko Santiago Bernabeu, Mabingwa Watetezi wa Ulaya, Real Madrid, wako kwao kurudiana na Schalke ya Germany ambayo waliitandika Bao 2-0 katika Mechi yao ya kwanzo huko Nchini Ujerumani.
Real
wako kwenye nafasi murua kuwa Timu ya kwanza kutua Robo Fainali ya
Mashindano haya kwani Mechi nyingine inayochezwa Jumanne Usiku ipo huko
Ureno kati ya FC Porto na FC Basel ambazo zilitoka 1-1 katika Mechi yao
ya kwanza huko Uswisi.
Jumatano
Usiku, Machi 11, pia zipo Mechi 2 za Marudiano za Raundi hii kati ya
Bayern Munich na FC Shakhtar Donetsk, zilizotoka 0-0 huko Ukraine,
ambayo itachezwa Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany na nyingine
ni ile itakayochezwa Stamford Bridge Jijini London kati ya Wenyeji
Chelsea FC na Paris Saint-Germain ambazo zilitoka 1-1 huko Paris,
France.
Mechi
za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONS LIGI
zitakamilika Wiki ijayo kwa Mechi 4, mbili Jumanne Machi 17 na mbili
Jumatano Machi 18.
RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 RATIBA
MARUDIANO
Jumanne 10 Machi 2015
FC Porto vs FC Basel 1893 [1-1]
Real Madrid CF vs Schalke 04 [2-0]
Jumatano 11 Machi 2015
Bayern Munich vs FC Shakhtar Donetsk [0-0]
Chelsea FC vs Paris Saint-Germain [1-1]
0 maoni:
Chapisha Maoni