Mbunge
wa jimbo la Kahama James Lembeli (kulia) akiwa na waziri mkuu Mizengo
Pinda ambaye leo anazuru eneo lililokubwa na tukio hilo.
Salaam za rambirambi
zimeendelea kumiminika kutoka sehemu mbalimbali nchini, kufuatia maafa
ya mvua ya mawe yaliyokikumba kijiji cha mwakata wilayani kahama mkoani
Shinyanga ambapo watu 42 wamepoteza maisha na wengine 91 kulazwa
hospitalini kwa matibabu.
Mbunge wa jimbo la
kahama James Lembeli akiwa safarini kikazi nchini Ethiopia, amempa pole
mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel
Maige kwa kufikwa na janga hilo kubwa na la kihistoria wilayani humo.
Akiwasiliana na Dunia
Kiganjani Blog kwa njia ya mtandao Lembeli amesema amepokea taarifa za
msiba huo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa watu wa mwakata amekuwa nao
karibu na wanampenda huku na yeye anawapenda.
Lembeli amesisitiza,
pamoja na kuwa safarini nje ya nchi lakini yuko pamoja na wale wote
waliofikwa na maafa hayo; kwa kuwaombea marehemu wapate pumziko la amani
na Mwenyezi mungu awarejeshee majeruhi afya yao haraka.
Wakati huhohuo, Mazishi ya miili ya watu 42 waliopoteza maisha kwenye janga hilo yamefanyika huku kasoro baadhi zikijitokeza.
Mpesya amesema katika
familia moja (jina halikutajwa), iliyopotelewa na watoto watatu wa kike
na wawili wa kiume imeghafilika na kuwazika marehemu pamoja, katika
makaburi mawili kwa kufuata jinsi ya me na ke.
Amesema, yeye kama
kiongozi ameamru mazishi hayo yafanyike upya kesho asubuhi, kwani mira
na desturi za kiafrika zinaelekeza kila mwili unapaswa kuzikwa kwenye
kaburi lake; na siyo kuchanganywa na mwili mwingine hata kama ni ndugu.
Mvua kubwa ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali na mafuliko imenyesha usiku wa kumkia leo
katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama na kusabisha
vifo vya watu na mifugo, huku familia zaidi ya 500 zikiachwa bila
makazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni