.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 14 Machi 2015

Tagged Under:

TANZANIA JANA YAPIGWA 6-2 NA MISRI BEACH SOCCER

By: Unknown On: Jumamosi, Machi 14, 2015
  • Share The Gag

  • IMG_20150313_160039Na Amplifaya Amplifaya
    Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania katika michuano ya ufukweni leo imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kukubali kichapo kikali cha goli 6-2.
    Walikuwa ni Tanzania ambao walianza mchezo katika morali nzuri ila mashambulizi yakiwa ya kushtukiza katika fukwe hizo za Escape One walifanikiwa kupata bao la kwanza kipindi cha kwanza na mfungaji akiwa ni Ally Rabbi.
    Haikuchukua muda mrefu sana mchezaji Mwalimu Akida aliwainua mashabiki waliokuwepo katika fukwe hizo mara baada ya kujipatia timu hiyo goli la pili na kuwafanya Tanzania waongoze kwa goli hizo 2.IMG_20150313_162417
    Waarabu wa Misri walirejea vizuri wakiwa kama wanacheza kwenye uwanja wao walimiliki mpira kwa asilimia kubwa zaidi huku wakifanya mashambulizi makali zaidi pia wakikosa magoli mengi.
    Misri walifunga bao lao la kwanza kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wao Islam Ahmed,  mapema baada ya kupata bao hilo waliendelea kujituma zaidi na hatimaye kupata bao lingine lililofungwa na Yehia Ally ambaye alifunga goli 4 peke yake leo, Goli jingine lilifungwa na Mohammed likiwa ni goli la 4 huku msumali wa mwisho ulimaliziwa na Yehia Ally na kukamilisha idadi ya mabao 6-2 kutoka kwa waarabu hao.
    Tanzania sasa inabidi ijiandae kikamilifu kwenda kupambana na Mafarao hao wa Misri nchini kwao baada ya wiki moja.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni