Dakika
90 zimemaliza Arsenal wakiwa na Ushindi wa bao 2-1, bao la Ushindi
likifungwa na Danny Welbeck mchezaji wa zamani wa Timu ya Manchester
United katika dakika ya 61 baada ya Valencia kufanya makosa ya kurudisha
mpira nyuma.
2-1
Ushindi!!
Umetupa bao!!
Umerudi na kuua!!
Danny Welbeck baada ya kutupia nyavuni bao la pili.
Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 25 la Nacho Monreal na Wayne Rooney kusawazisha Dakika ya 29 lakini Welbeck kuipa ushindi Arsenal katika Dakika ya 61.
Nje!! Di Maria
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Angel Di Maria kulambwa Kadi za Njano mbili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu. Huu ulikuwa Usiku mwema kwa Arsenal ambao wameendelea kutetea vyema Kombe la FA CUP ambalo wao ni Mabingwa Watetezi na pia wamekuwa wakiteswa na Man United kwa kufungwa Mechi 11 kati ya 15 zilizopita.
Unamvuta Mwamuzi jezi???Mhhh !! Hii ni La Liga EPL??
Kaa mbali kwanza!
Unakosea Di Maria ...tulia!! Rooney akituliza Jazba!!
Pia
kwenye Droo ya Nusu Fainali ya FA CUP, iliyofanyika maraa baada ya
Mechi hii, Arsenal watacheza na Mshindi kati ya Bradford City au Reading
ambao Juzi walitoka 0-0 kwenye Mechi yao ya Robo Fainali. Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Mshindi wa Liverpool na Blackburn Rovers, ambao nao walitoka 0-0, dhidi ya Aston Villa.
Kipindi cha pili Danny Webeck mchezaji wa zamani wa Man United aliipa bao la pili Arsenal katika dakika ya 61 na kufanya 2-1.
Rooney akisawazisha bao kipindi cha kwanza
Rooney baada ya kuisawazishia United bao kwa kufanya 1-1 dhidi ya Arsenal katika kipindi cha kwanza. Mpaka mapumziko kipindi cha kwanza Manchester United 1-1 Arsenal.
Nacho
Monreal dakika ya 25 kipindi cha kwanza kaifungia bao Arsenal nao Man
United walifufuka na dakika ya 29 Wayne Rooney aliisawazishia bao
Manchester United kwa kichwa na kufanya 1-1.
VIKOSI:Man United 11: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Di Maria, Fellaini, Young, Rooney
Akiba: Valdes, Rafael, Jones, Carrick, Januzaj, Mata, Falcao
Arsenal 11: Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Ozil, Sanchez, Welbeck
Akiba: Martinez, Gibbs, Chambers, Ramsey, Giroud, Walcott, Akpom
Man United vs Arsenal
0 maoni:
Chapisha Maoni