Luis
Suarez akishangilia vikali baada ya kuishindilia bao la Ushindi Real
Madrid na kuipatia Ushindi wa El Clasico Barcelona wa bao 2-1 leo huko
Camp Nou.
Kipindi cha pili dakika ya 56 Luis Suárez aliifungia bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Real baada ya kupata mpira kutoka kwa Daniel Alves. Ushindi huu umeipaisha Barcelona juu kileleni wakiwa na pointi 68 nyuma ya pointi 4 Real Madrid ambao mpaka sasa wamebakia nafasi ya pili wakiwa na pointi 64. Valencia ambaye yupo nafasi ya tatu anapointi 60 nae nyuma ya pointi 4 kuikama ta Real.
Ronaldo akioneshwa kadi ya njano
Ronaldo akipongezwa..
Ronaldo akishangilia bao lake la kusawazisha
Ronaldo aliisawazishia bao RealDakika ya 31 Cristiano Ronaldo aliisawazishia bao Real na kufanya 1-1akilishwa mpira na Karim Benzema.
Baadhi ya Wachezaji wa Barca wakimpongeza mwenzao baada ya kuifungia bao
Sergio Ramos aipagawa baada ya Jeremy kuwaua bao la kwanza...
Mpaka ndani ya nyavu za Real
Jérémy Mathieu akiwaua Real bao kwa kichwa!
Pepe baada ya kumwangusha chini Neymar
Gareth Bale akituliza mpira kiuzuri!
Cristiano Ronaldo akimiliki mpira.
Bale akiendesha mpira kipindi cha kwanza.
Bale akikimbizwa na Neymar
Kikosi cha Barcelona
Kikosi cha Real Madrid
Mwamuzi wa kati ni Antonio Miguel Mateu Lahoz na Mashabiki waliongia kuuona mtanange huu ni 99,000.
BARCELONA XI: Bravo, Alves, Pique, Mathieu, Alba, Rakitic, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar
AKIBA: Ter Stegen, Busquets, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Adriano.
REAL MADRID XI: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, Isco, Bale, Benzema, Ronaldo
AKIBA: Keylor Navas, Varane, Arbeloa, Illarramendi, Lucas Silva, Jese, Chicharito.
0 maoni:
Chapisha Maoni