UONGOZI
 wa Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park umetoa mwaliko kwa Vijana wote na 
Watanzania kwa ujumla kwenda kutumia Eneo hilo jipya na la kisasa 
kabisa. 
Ndani
 ya Eneo hilo upo Uwanja mkubwa wa kisasa wenye Kapeti la 3G pamoja na 
Kiwanja cha kucheza Mechi za Timu za Wachezaji Watano dhidi ya Watano, 
upo Uwanja wa Mpira wa Vikapu, Mpira wa Mikono na wa Magongo. Viwanja vyote vina Taa za kutumika Usiku na yapo ya Majengo ya Menejimenti pamoja na Vyumba vya Kubadilishia Jezi.
Akitangaza mwaliko huu kwa Vijana, Afisa Mwandamizi wa Utawala, Ismail A. Shah, amesema Timu ambazo zitahitaji kufanya mazoezi au kucheza Mechi kwa Kipindi cha kuanzia Saa 1 Usiku hadi Saa 4 Usiku, zipeleke maombi na majina kamili ya Wachezaji/Washiriki.
Kwa maelezo zaidi Waombaji wametakiwa kuwasiliana na Namba ya Simu 0714436347.
0 maoni:
Chapisha Maoni