Msanii
Vanessa Mdee akitoa burudani kwa madiva wa jiji la Mbeya wakati wa
Tamasha la Trust “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika jijini humo
katika ukumbi wa Mtenda Sunset uliopo Soweto lengo la Tamasha likiwa ni
kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa akina dada na mama wa jiji hilo.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Katikati) akiwajibika jukwaani
mbele ya umati wa akina dada waliojitokeza kwenye Tamasha la “Divas Only
Concert” ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Mtenda, Sunset-Soweto
jijini Mbeya. burudani hiyo ya nguvu iliandaliwa na chapa ya Trust toka
shirika lisilokuwa la kiserikali la DKT International ambalo
liliwakutanisha madiva kutoka sehemu mbalimbali wengi wao wakiwa ni
wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu juu ya
uzazi wa mpango.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee akiimba katikati ya mashabiki
wake wakati wa Tamasha la “Divas Only Concert” lililoandaliwa na chapa
ya Trust toka DKT International ambalo lilifanyika jijini Mbeya mwishoni
mwa wiki.
Mbeya
TRUST imeendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hususani wakina dada
katika mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya “Divas Only” ambapo kwa
wikiendi hii ilikua ni zamu ya jiji la Mbeya baada ya Tamasha hilo
kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kama
ilivyo ada Tamasha hilo humshirikisha Diva wa nguvu na msanii wa muziki
wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye alizikonga nyoyo za mashabiki wake
vilivyo. Tamasha hilo liliwavutia madiva kibao kutoka maeneo ya karibu
pamoja na vyuo mbalimbali vya jijini Mbeya kama TECU, Mzumbe, CBE na TIA
ambapo kiingilio cha Tamasha hilo kilipangwa kuwa Tsh. 10,000/= tu.
Trust
ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na
bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya
wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya
baadaye. Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili
ya mafanikio; Trust ipo hapa kukusaidia wakati wa safari hii.
“Kwa
mara nyingine ilikuwa ni fursa nzuri ya kufurahi kwa muda tuliopata wa
kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa jijini Mbeya na kufurahi na
kuelimishana, tumejifunza kutoka kwa wataalamu mambo mengi na njia
nyingi bora, kwamfano njia ya Kitanzi ni bora sana ina ufanisi wa zaidi
ya asilimia 99.9 na pia ni bora sana kwakua aina nyingi hazina vichocheo
”…
0 maoni:
Chapisha Maoni