.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 10 Desemba 2015

Tagged Under:

Emmanuel Okwi anarudi Simba

By: Unknown On: Alhamisi, Desemba 10, 2015
  • Share The Gag

  • Stori za Okwi kutaka kurudi Simba ambayo amewahi kuitumikia kwa vipindi viwili tofauti, ziliandikwa sana katika magazeti, kitu ambacho kilikuwa kinaaminika na wengi kutokana na uongozi wa Simba kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi, December 10 makamu wa Rais wa Simba Geofrey Kaburu amefunguka haya. Ni kweli wana mipango ya kumrejesha Okwi?
    ????????????????????????????????????

    “Sisi kwa maana ya uongozi wa klabu ya Simba kwa suala la usajili tumeshakamilisha na majina yamepelekwa TFF, ukweli wa Okwi ni kwamba hakuna mazungumzo rasmi ya uongozi juu ya kurudi kwa Emmanuel Okwi, hayo ni maneno mnayosikia pembeni hayo ni romours, kuhusu kufanya mawasiliano yapo ya kawaida yaani ya kirafiki kwa sababu haikatazwi ila kurudi Simba kwa mkataba mpya hilo halipo mezani kwa upande wetu” >>> Kaburu
    Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2o13 kwenda katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola 300000 ila baadae alivunja mkataba wake na klabu hiyo na kurudi kwao Uganda baada ya kushindwa kumlipa mshahara wake, baadae akaja Yanga na kurudi Simba na July 10 2015 Simba ilimuuza kwenda klabu ya Sonderjyske ya Denmark.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni