.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 11 Desemba 2015

Tagged Under:

Mwaka mmoja baada ya kupigwa risasi kwa golikipa wa Afrika Kusini, huyu ni staa mwingine aliyeuwawa kwa risasi …

By: Unknown On: Ijumaa, Desemba 11, 2015
  • Share The Gag

  • Mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Olimpia na Rangers ya Scotland ameuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa katika Parking za magari jijini La Ceiba Honduras, Arnold Peralta alikuwa likizo nyumbani kwao Honduras.
    Kifo cha Arnold Peralta ambaye anamudu kucheza nafasi ya kiungo kwa ufasaha kinachunguzwa na maafisa usalama wa nchi hiyo, ila taarifa za awali zinaonesha kuwa Arnold Peralta alipigwa risasi sio na majambazi ila inasadikika ni watu wenye visasi lakini tukio bado linachunguzwa.
    Olympics+Day+2+Men+Football+Spain+v+Honduras+ENz_YKSG4G9l
    Headlines za kifo cha Arnold Peralta kupigwa risasi zinakuja ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka auwawe kwa risasi golikipa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa, ambaye nae alipigwa risasi na majambazi ambao walienda kufanya uharifu katika nyumba ya mpenzi wake.
    TL_1081310-602x400
    Senzo Meyiwa

    0 maoni:

    Chapisha Maoni