Mwanakamati
wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of
Churches) Mchungaji Mchungaji Olivia Mallonga (kulia) akichangia mada
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22
Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu
maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua
maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John
Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua
hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa hayo Askofu Godfrey
Malassy.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of
Churches) Askofu Godfrey Malassy akionyesha kitabu mbele ya Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) kilichozinduliwa na Jumuiya ya Makanisa hayo
kinachohusu siri ya amani kwa taifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni