.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 7 Desemba 2015

Tagged Under:

Baada ya kipigo cha Chelsea, Jose Mourinho akiulizwa swali kuhusu kufanya usajili atakujibu hivi …

By: Unknown On: Jumatatu, Desemba 07, 2015
  • Share The Gag


  • Klabu ya Chelsea ya Uingereza usiku wa December 5 ilicheza mchezo wake wa 15 katika Ligi Kuu Uingereza dhidi ya klabu ya AFC Bournemouth katika dimba lake la Stamford Bridge, mchezo ambao ulimalizika kwa Chelsea kukubali kipigo cha goli 1-0 na kufanya ifikishe jumla ya mechi 8 ilizopoteza msimu huu.
    Baada ya kipigo hicho swali ambalo aliwahi kuulizwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuhusu usajili limerudi tena, wengi mwenendo wa matokeo mabovu wa Chelsea wanauhusisha na usajili, ila Mourinho amesimamia msimamo wake kuwa hawezi kumwambia mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich atoe fedha kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo la January.
    mourinho
    ” Kwa mara nyingine na jibu tena sina haja ya kuomba klabu ifanye usajili wa wachezaji, tulianza msimu tukiwa na hiki kikosi na wachezaji walitakiwa kuwa bora, hakuna haja ya kuomba klabu ifanye usajili katika dirisha dogo zaidi ya wachezaji waliopo kuimarisha viwango vyao”

    0 maoni:

    Chapisha Maoni