.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 13 Desemba 2015

Tagged Under:

TP Mazembe yapokea kipigo klabu Bingwa Dunia, Samatta na Ulimwengu kwenye rekodi hii

By: Unknown On: Jumapili, Desemba 13, 2015
  • Share The Gag


  • Michuano ya klabu Bingwa Dunia ilianza December 10 2015 katika ardhi ya Japan, hii ni michuano ambayo inatafuta Bingwa wa Dunia kwa ngazi ya vilabu, kwa upande wa bara la Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio ilikuwa inawakilisha bara hili.
    Generated by IJG JPEG Library
    TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ilianza kucheza michuano hiyo December 13 katika hatua ya robo fainali dhidi ya klabu ya Sanfrecce na kukubali kipigo cha goli 3-0, huu ni mchezo ambao watanzania wengi walikuwa wanautazama, kwani Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu  wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo.
    Generated by IJG JPEG Library
    Sanfrecce walianza kupata goli la kwanza dakika ya 44 kupitia kwa Shiotani ikiwa ni dakika moja imesalia kabla ya kwenda mapumziko. TP Mazembe walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha ila dakika ya 56 kipindi cha pili Chiba akapachika goli la pili kwa Sanfrecce, licha ya TP Mazembe kutokata tamaa, goli la dakika ya 78 la Asano ndio lilihitimisha safari ya TP Mazembe kwenda hatua ya nusu fainali.
    Generated by IJG JPEG Library
    Generated by IJG JPEG Library

    0 maoni:

    Chapisha Maoni