.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 8 Desemba 2015

Tagged Under:

FA CUP, DROO YA RAUNDI YA 3 YAPANGWA! MABINGWA ARSENAL KUKIPIGA NA SUNDERLAND NYUMBANI EMIRATES, MAN UNITED v SHEFFIELD UNITED, CHELSEA v LEYTON ORIENT/ SCUNTHORPE.

By: Unknown On: Jumanne, Desemba 08, 2015
  • Share The Gag

  • DROO ya Raundi ya 3 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini, imefanyika Usiku huu ikihusisha Timu zote za Ligi Kuu England na Daraja la Championship ambazo huanzia hapa.
    Droo hii, ambayo imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe, imefanyika huko Sport Wales National Centre Mjini Cardiff, na kuhusisha Timu 64 na Mechi zake zitachezwa kati ya Ijumaa Januari 8 na Jumatatu Januari 11.

    Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Mshindi kati ya Timu za Madaraja ya chini Leyton Orient v Scunthorpe United.
    Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.
    Liverpool wako Ugenini kuivaa Exeter City huku Mechi tamu iko White Hart Lane ambako Tottenhma watavaa Vinara wa Ligi Kuu England Leicester City. 

    Droo ya Raundi ya Tatu:
    Watford v Newcastle
    West Brom v Bristol City
    West Ham v Wolves
    Salford/Hartlepool v Derby
    Exeter City v Liverpool
    Northampton Town v MK Dons
    Peterborough v Preston
    Colchester v Charlton
    Tottenham v Leicester
    Arsenal v Sunderland
    Ipswich Town v Portsmouth
    Newport County v Blackburn Rovers
    Sheffield Wednesday v Fulham
    Wycombe Wanderers v Aston Villa
    Birmingham City v AFC Bournemouth
    Oxford United v Swansea City
    Brentford v Chesterfield or Walsall
    Bury v Bradford City
    Manchester United v Sheffield United
    Everton v Dagenham and Redbridge/Whitehawk
    Southampton v Crystal Palace
    Carlisle United v Yeovil Town
    Nottingham Forest v QPR
    Eastleigh v Bolton Wanderers
    Chelsea v Leyton Orient/Scunthorpe United

    0 maoni:

    Chapisha Maoni