Zipo habari zinazodai kuwa Louis van Gaal atapewa Mechi 2 zijazo kurekebisha mwelekeo wa jahazi lakini zipo dalili pengine hata huo muda haupo.
Balaa
kwa Louis van Gaal lilianza mara baada ya kuifunga Watford Bao 2-1 hapo
Novemba 21 na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu England lakini tangu wakati
huo hawajashinda hata Mechi 1 katika 6 walizocheza na kujikuta wakipigwa
mara 3 mfululizo na pia kung’olewa kwenye 4 Bora ya Ligi.
MAN UNITEDMechi zijazo za Ligi:
Desemba 26: Stoke City vs Man United
Desemba 28: Man United vs Chelsea
Januari 2: Man United vs Swansea City
Zipo
tetesi kuwa hata Wachezaji wa Man United, hasa wale Maveterani,
hawafurahishwi na uongozi wa Van Gaal huku Wachambuzi wengi wakidai
Mdachi huyo sasa amepitwa na wakati na kinachomweka juu tu ni sifa zake
alizozoa nyuma kwenye Historia yake. Wapo wanaosema Van Gaal atang’oka na Msaidizi wake Ryan Giggs kupewa ukaimu hadi mwishoni mwa Msimu na Giggs akifanya vizuri katika kipindi cha ukaimu hapo ndipo atakuwa wa kudumu .
Lakini pia zipo taarifa zinazodai Jose Mourinho, alietimuliwa na Chelsea Alhamisi iliyopita, ndie atashika wadhifa wa Umeneja wakati wowote kuanzia sasa.
Hadi sasa hamna mwenye uhakika nini kitajiri Man United na Klabu yenyewe haijazungumza chochote kama kawaida yao.
Wapo
Wachambuzi wanaokumbushia jinsi David Moyes alivyotimuliwa Msimu wa
2013/14 ingawa dalili zilikuwepo kwa muda kwamba anaishi kwa Siku za
kuhesabika lakini aliachwa kwenye wadhifa hadi Mwezi Aprili ilipofikia
hatua kuwa Man United hawatafuzu tena 4 Bora na hivyo kutocheza UEFA
CHAMPIONS LIGI na ndipo akafukuzwa.
Hadi sasa, kwa Man United, ndoto ya kumaliza ndani ya 4 Bora bado ipo hai lakini nani atakubali kila kukicha ni vipigo tu?
0 maoni:
Chapisha Maoni