.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 8 Desemba 2015

Tagged Under:

MASHABIKI WA MAN UNITED WALILIA UBUTU WA TIMU YA VAN GAAL! WAMWANDAMAKWA SARE!

By: Unknown On: Jumanne, Desemba 08, 2015
  • Share The Gag

  • BAADA ya Sare nyingine tena ya 0-0 hiyo jana Uwanjani Old Trafford waliyotoka na West Ham na kuporomoka hadi Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, Louis van Gaal amejikuta akishambuliwa vibaya na Mashabiki wa Manchester United kwenye Miatandao ya Kijamii.

    Kwenye Mtandao wa Twitter, Mashabiki wa Man United wamedai Van Gaal, Meneja wa Man United, anaivuruga Timu yao na kuiharibu Historia yao.

    Hivi karibuni, Man United wamekuwa wakipata shida kufunga Mabao na tangu waichape Everton 3-0 huko Goodison Park hapo Oktoba 17 kwenye Ligi, zikafuata Sare za 1-1 na CSKA Moscow kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Sare 3 za 0-0 na Man City, Middlesbrough, kwenye Capital One Cup ambayo walitolewa kwa Penati 3-1 na Crystal Palace kwenye Ligi.

    Baada ya hapo wakazifunga CSKA Moscow 1-0 kwenye UCL, WBA 2-0 kwenye Ligi, Watford 2-1 kwenye Ligi na kuanza Sare nyingine za 0-0 na PSV kwenye UCL, 1-1 na Leicester kwenye Ligi na hii 0-0 na West Ham.
    0 comments

    0 maoni:

    Chapisha Maoni