.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 9 Februari 2015

Tagged Under:

WAKALA JORGE MENDES: DAVID DE GEA KWENYE MAONGEZI DILI MPYA NA KLABU YA MASHETANI WEKUNDU MAN UNITED.

By: Unknown On: Jumatatu, Februari 09, 2015
  • Share The Gag

  • Kipa Nambari Wani wa Manchester United David De Gea, yupo kwenye mazungumzo na Klabu yake kuhusu kupewa Dili mpya na wala hajafikia makubaliano na Real Madrid kuhamia huko Spain. 
    Habari hizi zimetobolewa na Wakala wa Kipa huyo kutoka Spain, Jorge Mendes, ambae ametupilia mbali dhana kuwa amekubaliana na Real Madrid kujiunga nao.
    Hivi sasa De Gea, mwenye Miaka 24 na ambae pia ni Kipa wa Timu ya Taifa ya Spain, amebakiza kama Miezi 18 kwenye Mkataba wake na Man United na hilo lilianzisha uvumi mkubwa kuwa ataenda Real Madrid.
    Akiongea na Kituo cha Redio Cadena Ser hapo Jana, Jorge Mendes, alisema: “Hivi sasa tupo kwenye mazungumzo na Man United kumpa Mkataba mpya lakini hatujasaini! Hamna ukweli kwamba yapo makubaliano kujiunga na Real!”
    De Gea ni Mzaliwa wa Jiji la Madrid na alianza kuichezea Atlético Madrid tangu akiwa na Miaka 13 kisha kuichezea Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza Mwaka 2009 na Mwaka uliofuatia alikuwa langoni wakati Atletico inatwaa UEFA EUROPA LIGI na UEFA SUPER CUP.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni