.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 26 Februari 2015

Tagged Under:

Tanzania kushiriki mashindano ya kuogelea kanda ya 4

By: Unknown On: Alhamisi, Februari 26, 2015
  • Share The Gag


  • photos.demandstudios.com-getty-article-197-91-87788991_XS
    Na Amplifaya Amplifaya
    KOCHA wa timu ya Taifa ya Kuogelea, Alex
    Mwaipasi amesema Tanzania inatarajiwa
    kushiriki kwenye mashindano ya Kanda ya Nne
    yaliyopangwa kufanyika nchini Angola, Mei
    mwaka huu.
    Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika
    ilikuwa ni mwaka jana nchini Uganda ambapo
    Tanzania iliwakilishwa na wachezaji kadhaa
    waliofanya vizuri wakiwamo Hilal Hilal na Sonia
    Tomiotto.
    Akizungumza jana, Mwaipasi
    alisema katika kuhakikisha wanafanya vizuri
    katika mashindano ya mwaka huu, tayari
    wameshaanza mchakato wa kusaka kikosi bora.
    “Tumeanza mchakato wa kuwatafuta wachezaji
    bora kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha,
    Morogoro na Dar es Salaam na tuna imani
    mambo yatakuwa mazuri tutakapoanza kambi
    baadaye,” alisema Mwaipasi.
    Alisema wachezaji hao watafuatiliwa mwenendo
    wao katika mashindano ya kitaifa
    yatakayofanyika mwezi ujao, na mashindano ya
    wazi ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika
    Kusini.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni