Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui ushindi katika mchezo huo wa fainali.
Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni 2.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.
0 maoni:
Chapisha Maoni