.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 17 Februari 2015

Tagged Under:

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO JUMATANO SCHALKE 04 vs REAL MADRID,

By: Unknown On: Jumanne, Februari 17, 2015
  • Share The Gag


  • LEO Jumatano Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI Real Madrid wanarudi tena Veltins-Arena, Mjini Gelsenkirchen huko Germany ambako Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliwanyuka Wenyeji wao Schalke 6-1.
    Hata hivyo safari hii Schalke wako chini ya Meneja wa zamani wa Chelsea aliewabebesha Kombe hili Mwaka 2012 Roberto Di Matteo lakini wana kibarua kigumu kwani pia atawakosa Nyota wake Majeruhi Julian Draxler, Leon Goretzka na Jefferson Farfan.
    Lakini pia Real, chini ya Meneja Carlo Ancelotti wana Majeruhi ambao ni pamoja na Viungo wao muhimu James Rodriguez na Luca Modric na Beki Sergio Ramos ingawa Beki mwingine, Pepe, amepona na huenda akacheza.
    Katika Mechi nyingine ya Jumatano, Mabingwa wa Uswisi FC Basel, ambao waliwapiku na kuwatupa nje ya Mashindano haya Liverpool katika hatua za Makundi, wanaivaa Porto ya Ureno ambayo haikufungwa hata Mechi kwenye hatua hiyo ya Makundi.

    RATIBA LEO JUMATANO
    Jumatano 18 Februari 2015

    Schalke 04 vs Real Madrid CF
    FC Basel 1893 vs FC Porto
    Jumanne 24 Februari 2015
    Juventus FC vs BV Borussia Dortmund
    Manchester City vs FC Barcelona
    Jumatano 25 Februari 2015
    Arsenal FC vs AS Monaco FC Bayer 04 

    Leverkusen vs Atletico de Madrid

    0 maoni:

    Chapisha Maoni