.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 30 Juni 2016

Tagged Under:

Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta

By: Unknown On: Alhamisi, Juni 30, 2016
  • Share The Gag

  • Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Petro Marwa kwenye  maonesho ya  kimataifa ya  sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es  Salaam.
    Mhandisi Petro alisema kumekuwepo na dhana  kuwa  wawekezaji kutoka nje ya nchi wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi na mafuta  jambo ambalo si sahihi.Alisema ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji kwenye  sekta za  gesi na mafuta,  Serikali imeweka sheria nzuri za kuwezesha watanzania kuwa sehemu  ya uchumi wa gesi na mafuta.
    “ Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka  2015 kifungu cha  218 kinaeleza ushiriki wa serikali  kupitia Kampuni ya  Mafuta ya  Taifa (National Oil Company) na kifungu cha  219  na 220 kinaainisha ushiriki  wa watanzania katika utoaji wa  huduma na bidhaa kwa makampuni yaliyowekeza nchini kwenye  sekta za mafuta na gesi,” alisema  Mhandisi Petro.
    Mhandisi Petro aliendelea kusema kuwa  serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji  kwenye uvunaji wa rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili na kuchangia  katika ukuaji wa uchumi  wa nchi.
    D1 
    Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia wateja katika  Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
    D2 
    Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kulia) kutoka  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
    D3 
    Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo  (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara  kwa mteja aliyetembelea banda  hilo  katika Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
    D5 
     Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    D7 
    Neema Mwambenja kutoka Taasisi ya  Environmental Foundation for  Tanzania (EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) (katikati) akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye banda la  REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana Magige kutoka  taasisi hiyo.
    D8 
    Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman Khalid (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Afisa Usalama na Mazingira kutoka  shirika hilo Paul Thobias.
    D6 
    Banda la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama linavyoonekana pichani  kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
    ———————————————
    Akielezea mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati na Madini  ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu mafuta na gesi katika  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini (MRI).
    Aliongeza kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha  wanafunzi wanaofanya  vizuri katika masomo  ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni