Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na
wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi
bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium
nchini Tanzania, ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la
Tanzania.
Wakitoa
taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wamesema kuwa uhaba wa
gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari
ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu
zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya
kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa
wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka 2035. Mnamo mwaka
2010 Mwanafisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa
ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu
huo ulikuwa umesababisha na wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria
itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile
kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi
kuliko ile ya Oxygen.
Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema……..>>>”Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI”
0 maoni:
Chapisha Maoni