POLAND
imeingia Robo Fainali ya EURO 2016 baada ya kuitoa Switzerland kwa
Penati 5-4 kufuatia Sare ya 1-1 katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu
16 ya EURO 2016, iliyochezwa huko Stade Geoffroy Guichard Mjini St
Etienne. Mabao hayo yalidumu hadi Dakika 90 kumalizika na Dakika za Nyiongeza 30 hazikubadili kitu na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Poland walifunga Penati zao zote 5 lakini Switzerland walikosa Penati ya Pili iliyopigwa na Mchezaji Mpya wa Arsenal, Granit Xhaka.
Kwenye Robo Fainali, Poland watacheza na Mshindi kati ya Croatia na Portugal wanaocheza baadae Leo.
0 maoni:
Chapisha Maoni