Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima
kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate
Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto
Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima
iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha
televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika
kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema
(kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess
inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba
wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye
viwanja vya Karimjee.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni
Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija
ya kufuturisha Watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate
Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni
rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
serikali inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea
watoto yatima nchini na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha
wamiliki na vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam
katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princess
inayoandaa kipindi cha Mboni Show hafla iliyojumuisha watoto yatima 283
kutoka Vituo vitano vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea
watoto yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya
watoto hao na sio vinginevyo. Kuhusu malezi ya Watoto yatima, Makamu wa
Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu bora,upendo na si
kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali.
0 maoni:
Chapisha Maoni