.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 11 Januari 2017

Tagged Under:

PATA RATIBA NZIMA YA AFCON 2017: FAINALI KUANZA JUMAMOSI JAN. 14, 2017

By: Unknown On: Jumatano, Januari 11, 2017
  • Share The Gag


  • MASHINDANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yataanza Jumamosi Januari 14 huko Gabon na kushirikisha Nchi 16 zilizogawanywa Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

    AFCON, ambayo Fainali yake itakuwa Februari 5, itachezwa kwenye Viwanja Vinne vya Miji ya Libreville, Franceville, Oyem na Port Gentil.
    Viwanja vitakavyotumika ni Stade de l’AmitiĆ© huko Libreville, Gabon, unaochukua Watu 38,000, ambako Kundi A ndio litacheza Mechi zake, na kingine cha Kundi B ni Port Gentil Stadium, Port Gentil, wenye kuchukua Washabiki 20,000, Kundi C lipo Stade de Franceville Mjini Franceville wenye uwezo wa Watu 20,000 wakati Kundi D litakuwa huko Oyem Stadium ulioko Assok Ngomo, Gabon, uwezo 20,000.

    Mabingwa Watetezi wa Afrika ni Ivory Coast lakini safari hii watawakosa Wachezaji wao wakubwa, wale Ndugu Toure, yaani Yaya na Kolo, ambao wamestaafu, na Majeruhi Yao Gervinho.



    MAKUNDI:
    KUNDI A:
    Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea-Bissau
    KUNDI B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
    KUNDI C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
    KUNDI D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

    Ivory Coast walitwaa Ubingwa wa Afrika huko Equatorial Guinea Mwaka 2015.

    Wenyeji Gabon wapo Kundi A pamoja na Burkina Faso, Cameroon na Guinea-Bissau iliyotinga Fainali kwa mara ya kwanza.
    Jirani zetu Uganda wapo kundi D pamoja na Ghana, Mali na Egypt ambao wanarejea kwenye Fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu watwae Ubingwa Mwaka 2010.

    AFCON 2017RATIBA
    Mechi za Makundi
    Jumamosi Januari 14
    Kundi A

    1900 Gabon v Guinea-Bissau
    2200 Burkina Faso v Cameroon

    Jumapili Januari 15
    Kundi B

    1900 Algeria v Zimbabwe
    2200 Tunisia v Senegal

    Jumatatu Januari 16
    Kundi C

    1900 Ivory Coast v Togo
    2200 Congo DR v Morocco

    Jumanne Januari 17
    Kundi D

    1900 Ghana v Uganda
    2200 Mali v Egypt

    Jumatano Januari 18
    Kundi A

    1900 Gabon v Burkina Faso
    2200 Cameroon v Guinea-Bissau

    Alhamisi Januari 19
    Kundi B

    1900 Algeria v Tunisia
    2200 Senegal v Zimbabwe

    Ijumaa Januari 20
    Kundi C

    1900 Ivory Coast v Congo DR
    2200 Morocco v Togo

    Jumamosi Januari 21
    Kundi D

    1900 Ghana v Mali
    2200 Egypt v Uganda

    Jumapili Januari 22
    Kundi A

    2200 Cameroon v Gabon
    2200 Guinea-Bissau v Burkina Faso

    Jumatatu Januari 23
    Kundi B

    2200 Senegal v Algeria
    2200 Zimbabwe v Tunisia

    Jumanne Januari 24
    Kundi C

    2200 Morocco v­­ Ivory Coast
    2200 Togo v Congo DR

    Jumatano Januari 25
    Kundi D

    2200 Egypt v Ghana
    2200 Uganda v Mali

    Robo Fainali
    Jumamosi Januari 28

    1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa 2 Kundi B
    2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa 2 Kundi A

    Jumapili Januari 29

    1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa 2 Kundi D
    2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa 2 Kundi C

    Nusu Fainali
    Jumatano Februari 1

    2200 Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4

    Alhamisi Februari 2

    2200 Mshindi RF 2 v Mshindi RF 3

    Mshindi wa 3
    Jumamosi Februari 4

    2200 Aliefungwa NF 1 v Aliefungwa NF 2

    Fainali
    Jumapili Februari 5

    2200 Finalist 1 v Finalist 2

    NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
    -Egypt-Mara 7
    -Cameroon, Ghana-Mara 4
    -Nigeria-Mara 3
    -Congo DR-Mara 2
    -Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

    0 maoni:

    Chapisha Maoni