.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 9 Januari 2017

Tagged Under:

EMIRATES FA CUP – DROO RAUNDI YA 4 YAFANYIKA LEO: MABINGWA MAN UNITED vs WIGAN NDANI YA UWANJA WA OLD TRAFFORD, CHELSEA v BRENTFORD

By: Unknown On: Jumatatu, Januari 09, 2017
  • Share The Gag

  • DROO YA RAUNDI YA 4 ya EMIRATES FA CUP imefanyika Leo Usiku huko BT Tower Mjini London ikiendeshwa na Wachezaji wa zamani wa Kimataifa wa England Michael Owen na Martin Keown na Mabingwa Watetezi Manchester United kupangwa kucheza kwao Old Trafford na Wigan Athletics.

    Man City na Arsenal zote zimepangwa kucheza Ugenini kwa Arsenal kuivaa Southampton au Norwich na Man City kucheza na Mshindi kati ya Crystal Palace na Bolton.
    Liverpool, kama wataifunga Plymouth katika Mechi yao ya Marudiano baada ya Sare, watakuwa kwao Anfield kucheza na Wolves.
    Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wao wako kwao Stamford Bridge kuivaa Brentford.
    Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City, watacheza Ugenini na Derby County wakati Tottenham wakicheza Nyumbani White Hart Lane na Wycombe.
    Mechi 16 za Raundi ya 4 zitachezwa Wikiendi ya Januari 28 na 29.
    DROO KAMILI TIMU 16:
    Crystal Palace au Bolton v Manchester City
    Middlesbrough v Accrington Stanley
    Fulham v Hull City
    Blackburn v Barnsley au Blackpool
    Burnley au Sunderland v Fleetwood au Bristol City
    Rochdale v Huddersfield Town
    Millwall v Watford
    Manchester United v Wigan Athletic
    Chelsea v Brentford
    Lincoln au Ipswich v Brighton
    Southampton au Norwich v Arsenal
    Plymouth au Liverpool v Wolves
    AFC Wimbledon au Sutton v Cambridge au Leeds
    Oxford United v Newcastle au Birmingham
    Derby County v Leicester City
    Tottenham v Wycombe

    0 maoni:

    Chapisha Maoni