.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 11 Januari 2017

Tagged Under:

MAPINDUZI CUP: SIMBA YAITOA YANGA KWA MATUTA 4-2, FAINALI SASA NI AZAM FC vs SIMBA

By: Unknown On: Jumatano, Januari 11, 2017
  • Share The Gag
  • Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, iliyokuwa Bigi Mechi, Dabi ya Kariakoo iliyohamia Amaan Stadium Zanzibar. Ilichezwa Usiku na Simba na Yanga kutoka 0-0 katika Dakika 90 lakini Simba kuibuka kidedea kwa Mikwaju ya Penati 4-2 na kutinga Fainali watakayocheza na Azam FC.
    Katika Nusu Fainali nyingine iliyochezwa mapema Taifa Jang’ombe ya Zanzibar ilifungwa 1-0 na Azam FC kwa Bao la Dakika ya 33 la Frank Domayo.
    Kwenye Mechi ya Watani wa Jadi, Timu zote zilishambuliana kwa zamu ingawa Yanga walionekana kutawala zaidi bila matunda yeyote na Gemu kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.

    Katika Penati hizo, Simba walifunga kupitia Kepteni wao Jonas Mkude, Kipa Daniel Agyei, Muzamil Yasin na Bokungu wakati ile iliyopigwa na Mwanjali kuokolewa na Kipa wa Yanga Munishi.

    Penati za Yanga zilifungwa na Simon Msuva na Thabani Kamusoko na zile za Kipa Munishi na Mwinyi Haji ziliokolewa na Kipa wa Simba Daniel Agyei.

    Fainali ya Mapinduzi Cup itachezwa Ijumaa Januari 13.

    VIKOSI VILIVYOANZA:
    YANGA:
    Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke

    SIMBA:
    Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamil Yassin, Mohamed
    Ibrahim

    Mohamed Ibrahim akimtoka beki wa Yanga wakati mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, Simba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2

    Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akijaribu kumtoka beki wa Yanga Haji Mwinyi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi leo Usiku katika uwanja wa Amani, Simba wakifanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kushinda kwa penati 4-2­­
    KOMBE LA MAPINDUZI
    Ratiba/Matokeo:
    Desemba 30, 2016

    Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

    Januari 1, 2017
    KVZ 0 URA 2
    Simba 2 Taifa Jang'ombe 1
     

    Januari 2, 2017 Azam 1 Zimamoto 0
    Yanga 6 Jamhuri 0

    Januari 3, 2017
    Jang'ombe Boys 2 URA 1
    KVZ 0 Simba 1

    Januari 4, 2017
    Zimamoto 0 Yanga 2
    Jamhuri 0 Azam 0

    Januari 5, 2017
    KVZ 1 Jang'ombe Boys 3
    Simba 0 URA 0

    Januari 6, 2017
    Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

    Januari 7, 2017

    Jamhuri 0 Zimamoto 2
    Yanga 0 Azam 4

    Januari 8, 2017

    Simba 2 Jang'ombe Boys 0
    Taifa Jang'ombe 1 URA 0

    Januari 10, 2017
    Nusu Fainali

    Azam FC 1 Taifa Jang’ombe 0
    Simba 0 Yanga 0 [Penati 4-2]

    Ijumaa, Januari 13, 2017
    FAINALI

    Saa 2: 15 Usiku
    Azam FC v Simba

    0 maoni:

    Chapisha Maoni