.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 2 Desemba 2014

Tagged Under:

LIGI KUU ENGLAND KUENDELEA TENA LEO

By: Unknown On: Jumanne, Desemba 02, 2014
  • Share The Gag

  • MENEJA wa Manchester United Louis Van Gaal anaamini ni muhimu kabisa wimbi la ushindi kuendelea watakapocheza na Stoke City Uwanjani Old Trafford Jumanne Usiku katika Mechi ya Ligi Kuu England.
    Licha ya kukabiliwa na majeruhi kibao, Man United wapo Nafasi ya 4 kwenye Ligi baada ya kupata ushindi Mechi 3 mfululizo dhidi ya Crystal Palace, Arsenal na Hull City.
    Akiongea kwenye mahojiano kuhusu Mechi na Stoke City, Van Gaal amesema: “Ushindi kwa Klabu kubwa kama Man United ni Muhimu, natumai tutashinda dhidi ya Stoke. Lakini kwenye Ligi Kuu si kila kitu rahisi. Ukiwaona Liverpool wakihangaika kwa Dakika 85 na kufunga Bao moja inaonyesha hilo. Umewaona Arsenal wakisumbuka na West Bromwich kwenye Mechi ambayo wangeweza kufungwa. Ligi Kuu inafurahisha sana, hujui nini litatokea!”

    Hata hivyo, Van Gaal amekiri Old Trafford ni safi hasa baada ya Mashabiki wao kuamka na kuipa sapoti kubwa Timu yao.

    Kwenye Mechi hii, kila Timu itakosa Masta wao kadhaa ambao ni majeruhi kwa Man United kuwakosa Angel Di Maria. Luke Shaw, Daley Blind na Phil Jones wakati Stoke watawakosa Steve Sidwell, Glenn Whelan, Victor Moses, Robert Huth na Peter Odemwingie.


    RATIBA: LEO JUMANNE
    Jumanne Desemba 2 

    22:45 Burnley v Newcastle
    22:45 Leicester v Liverpool
    22:45 Man United v Stoke
    22:45 Swansea v QPR
    23:00 Crystal Palace v Aston Villa
    23:00 West Brom v West Ham


    KESHO JUMATANO.
    Jumatano Desemba 3 
    22:45 Arsenal v Southampton 
    22:45 Chelsea v Tottenham 
    22:45 Everton v Hull
    22:45 Sunderland v Man City

    0 maoni:

    Chapisha Maoni