.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 29 Novemba 2014

Tagged Under:

JACK WILSHERE NJE MIEZI 3!

By: Unknown On: Jumamosi, Novemba 29, 2014
  • Share The Gag

  • Arsenal Jack Wilshere atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa operesheni ya enka yake hii Leo.
    Wilshere aliumia Jumamosi iliyopita wakati Arsenal inachapwa Bao 2-1 na Manchester United Uwanjani Emirates.
    Habari hizi za operesheni ya Wilshere zimethibitishwa na Arsenal na mwenyewe Wilshere aliposti Picha yake Mtandaoni akiwa Kitandani baada ya kufanyiwa hiyo operesheni.

    Kukosekana kwa Wilshere ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo sasa imekumbwa na Majeruhi wengi baada ya pia Jumatano kupoteza Wachezaji wawili walioumia kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI walipoifunga Borussia Dortmund Bao 2-0.
    Wachezaji hao wawili ni Nahodha wao Mikel Arteta na Yaya Sanogo ambao watakuwa nje kwa muda abao unaweza kufikia hata Wiki 6.

    Majeruhi wengine wa Arsenal ni Mesut Özil, Theo Walcott, Danny Welbeck, Mathieu Debuchy, Abou Diaby, Wojciech Szczesny na David Ospina.
    Kuhusu balaa hilo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza: “Hali hii ya majeruhi ni tatizo kwani tuna Mechi nyingii.”

    0 maoni:

    Chapisha Maoni