.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 27 Desemba 2014

Tagged Under:

CHRISTIAN BELLA NA BENDI YAKE YA MALAIKA BENDI WATAKUWA KAHAMA USIKU WA LEO KUTOA BURUDANI NDANI

By: Unknown On: Jumamosi, Desemba 27, 2014
  • Share The Gag

  • Chini ya Uongozi wa Mtunzi na Mwimbaji Mahiri na mtunzi bora wa mwaka wa Kili Music Awards Christian Bella ilipotumbuiza mamia ya wapenzi wao katika ukumbi wa Raha Bukoba wa Lina's Night  Club akiwa sambamba na  Safu yake ya  ushambuliaji ya Malaika Band. 
    BENDI ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku huu ilitoa Burudani kali ya kukata na shoka kwenye ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba ikiwa ni kumalizia sikukuu za X-mass siku ya Boxing Day" na kuwapagawisha mashabiki kwa shoo kali na ya nguvu.
    Onyesho hilo lililoanza saa mbili usiku ambapo Malaika Bendi walikuwa wakiwapa ladha mashabiki kwa kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo zinazobamba.
    Ilipofika saa nne na nusu ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi hiyo Christian Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi Mapenzi ambao ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale ambao walikuwa wakinyemelewa na usingizi kuamka.
    Bella alizidi kuwapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo zinatamba katika redio na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani Kama Mama, Yako wapi Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
    Mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ akifanya yake usiku huu siku ya sikukuu Boxing Day kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club, Bukoba uliopo Bukoba mjini.
    Madansa wa Malaika Music bendi wakifanya yao.
    Christian Bella Christian Bella 'Obama' achengua mashabiki kwa kutoa Burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Lina's Night Club usiku huu wa Boxing Day' katika kumalizia sikukuu za x-mass na kusonga kuoona mwaka Mpya 2015.
    Wanenguaji wa Malaika Band wakiwajibika kwenye ukumbi wa Lina's Night Club usiku huu wa
    Boxing Day Ijumaa.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni