.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 21 Novemba 2014

Tagged Under:

MANCHESTER UNITED KUIPIKU ARSENAL! WAJIPANGA UPYA KUMNASA MATS HUMMELS MWEZI JANUARI

By: Unknown On: Ijumaa, Novemba 21, 2014
  • Share The Gag

  • Meneja wa Manchester United Louis van Gaal yupo mbioni ili kumpata Sentahafu wa Germany na Klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa kwa Ada ambayo itavunja Rekodi ya Uingereza kwa Beki. Man United walimlenga Hummels kabla Msimu huu kuanza lakini Dili hiyo ikashindikana lakini Makamu Mwenyekiti Mtendaji, Ed Woodward, anahisi sasa ni wakati muafaka kwani inaelekea Dortmund watalegeza msimamo wao na kukubali kumuuza.

    Hata hivyo, chimbuko la habari hizi zimedai ili kumpata Hummels itabidi Man United walipe zaidi ya Pauni Milioni 32 Dau ambalo litazidi lile la Man City walipolipa kiasi hicho kumnunua Eliaquim Mangala kutoka FC Porto mwanzoni mwa Msimu na kuweka Rekodi ya kuwa Beki ghali huko Uingereza. 
    Hivi sasa Hummels anadaiwa kushuka kiwango kile alichokionyesha alipoiwezesha Germany kutwaa Kombe la Dunia Mwezi Julai huko Brazil na hili hasa limekuja baada ya kukumbwa na majeruhi.

    Klabu ya Hummels, Dortmund, hivi sasa inasuasua kwenye Bundesliga ikiwa nafasi ya 4 toka mkiani ikiwa na Pointi 10 tu baada ya Mechi 11 za Ligi.

    Akiongea na Wawekezaji Jumanne iliyopita, Ed Woodward alitamka: “Hatuingii Sokoni kusaka viraka vya muda mfupi. Lakini tunao walengwa tunaowataka mwishoni mwa Msimu. Ikitokea yeyote kati yao atapatikana Januari, kitu ambacho adimu, sisi tutamchukua!”

    Ikiwa Hummels atapatikana, hilo litawasaidia sana Man United wenye Difensi dhaifu na Wachezaji wanaokumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kina Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans.

    Mbali ya Hummels, pia zipo taarifa kuwa Van Gaal anamnyemelea Kiungo wa Holland anaechezea AS Roma, Kevin Strootman, ambae hivi karibuni alirejea Uwanjani na kuingizwa kutoka Benchi wakati AS Roma inaichapa Torino 3-0 baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akijiuguza Goti lake

    0 maoni:

    Chapisha Maoni