Akiongea huko Aon Training Complex, Carrington Jijini Manchester, Van Gaal alitoboa kuwa Angel Di Maria, David De Gea na Michael Carrick wako fiti kuivaa Arsenal.
Alifafanua: “Di Maria amefanya mazoezi kawaida tu, hamna tatizo hapo lakini Shaw lipo. De Gea safi, hamna tatizo. Kwa Carrick inabidi tusubiri kidogo lakini yupo tayari kucheza.”
Kuhusu kuumia kwa Kiungo Daley Blind ambae alipata tatizo la Goti akiichezea Nchi yake Netherlands, Van Gaal amesema amewekewa sapoti kwenye Goti na atapimwa baada ya Siku 10 lakini hayupo katika hali mbaya kama ilivyofikiriwa.
Arsenal wataingia kwenye Mechi hii ya Jumamosi wakiwa Nafasi ya 6 Pointi 1 tu mbele ya Man United ambayo iko Nafasi ya 7.

Mara ya mwisho Arsenal kuifunga Man United ni Mei Mosi Mwaka 2011 Bao 1-0 Uwanjani Emirates kwenye Mechi ya Ligi na tangu wakati huo wamecheza Mechi 6 na kutoka Sare 2 tu na zote zilizobaki Man United kushinda ukiwemo ushindi wa kishindo wa Bao 8-2 hapo Tarehe 28 Agosti 2012.
Van Gaal akiteta jambo na Vijana wake leo Ijumaa
Wachezaji wa United wakijifua leo tayari kwa mchezo wao na Arsenal Emirates.
Kazi ipo kesho!
0 maoni:
Chapisha Maoni