.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 10 Novemba 2014

Tagged Under:

SWANSEA CITY 2 - 1 ARSENAL,

By: Unknown On: Jumatatu, Novemba 10, 2014
  • Share The Gag


  • Alexis Sánchez aliifungia bao Arsenal dakika ya 63
    Swansea City walifanya bidii na dakika ya 75 mchezaji G. Sigurdsson alisawazisha bao hilo kwa mpira wa adhabu wa frii kiki uliojaa moja kwa moja wavuni kwa kufanya 1-1. 
    B. Gomis aliwashona bao dakika ya 78 kwa mpira wa kichwa baada ya kupigwa kona na kufanya kuwa mbele ya bao 2-1 dhidi ya Arsenal.
    Alexis Sanchez (left) slides the ball home to give Arsenal the lead just after the hour markSanchez kiulaini akiifunga Swansea City bao na kufanya 1-0.Sanchez jumps for joy after putting Arsenal a goal up with a tidy finish from 12 yards
    Alexis Sanchez akishangilia bao lake
    Liberty Stadium Usiku huu ilikuwa ni nderemo baada ya wenye Nyumba Swansea City kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Arsenal Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

    Arsenal walipata Bao lao Dakika ya 63 baada ya Oxlade-Chamberlain kuunasa Mpira katikati ya Uwanja na kuwachambua Wapinzani wawili kisha kumpasia Cazorla ambae haraka alimpelekea Danny Welbeck na kumhadaa Beki mmoja na kumsogezea Alexis Sanchez aliefumua Shuti lililomshinda Kipa wa zamani wa Arsenal, Lukas Fabianski.

    Dakika ya 75, Swansea walisawazisha kwa Frikiki murua ya Gylfi Sigurdsson aliyopiga kutoka Mita 25 na kumshinda Kipa Szczesny.
    Frikiki hiyo ilitokana na Rafu ya Gibbs kwa Barrow.
    Swansea walipiga Bao la Pili Dakika ya 78 kupitia Bafetimbi Gomis ambae aliingizwa Dakika 1 tu nyuma kumbadili Wilfried Bony na kuugusa Mpira kwa mara ya kwanza tu.

    Bao hilo lilitokana na kazi njema ya Jefferson Montero aliempita Calum Chambers na kutumbukiza Krosi iliyopigwa Kichwa na Bafetimbi Gomis na kutinga wavuni.
    Ushindi huu umewapaisha Swansea hadi Nafasi ya 5 na kuwashusha Arsenal Nafasi ya 6.

    Ligi Kuu England sasa itakuwa nje kupisha Mechi za Kimataifa na Arsenal watarejea Uwanjani Jumamosi Novemba 22 wakiwa kwao Emirates kucheza na Manchester United.

    Chupuchupu wafungwe bao hapa Arsenal

    0 maoni:

    Chapisha Maoni