.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 18 Novemba 2014

Tagged Under:

ARSENE WENGER: ASEME HANA MPANGO WA KUMUUZA LUKAS PODOLSKI

By: Unknown On: Jumanne, Novemba 18, 2014
  • Share The Gag

  • MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza hana mpango wowote wa kumuuza Lukas Podolski baada ya Fowadi huyo wa Germany kudokeza anaweza kuondoka Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguka.
    Msimu huu, Podolski, mwenye Miaka 29, hajaanza hata Mechi moja ya Ligi Kuu England na ukosaji huo namba umemkera kiasi cha kudokeza ataondoka Arsenal kwenda kwingine.
    Moja ya Klabu zinazomtaka Podolski inadaiwa kuwa ni Napoli ya Italy na mwenyewe alipoulizwa hilo alijibu: “Chochote kinawezekana Siku hizi. Huwezi kukataa hilo!”

    Lakini Wenger amekataa kama hilo linaweza kutokea kwa kusisitiza: “Ni mimi ndie ninaepanga Bei na hiyo Ofa hailingani na thamani yake. Hauzwi na hamna Ofa!”

    Wenger alifafanua kuwa Podolski anachezea pozisheni yenye ushindani mkubwa na pia alichelewa kurudi Mazoezini kwa ajili ya Msimu mpya baada ya kupewa Likizo ndefu baada ya Germany kutwaa Ubingwa wa Dunia na hilo limeathiri Mazoezi yake kumfanya awe fiti.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni