.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 8 Januari 2016

Tagged Under:

RATIBA - FA CUP: KUENDELEA LEO IJUMAA LIVERPOOL vs EXETER, JUMAMOSI MITANANGE KIBAO KUPIGWA!

By: Unknown On: Ijumaa, Januari 08, 2016
  • Share The Gag

  • FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini na ni Kombe kongwe kabisa Duniani, litaanza kurindima Ijumaa Usiku huko England kwa Mechi pekee huko Mjini Exeter kati ya Exeter City FC na Liverpool.
    Huu ni mwanzo wa Mechi za Raundi ya 3 FA CUP, inayoshirikisha jumla ya Timu 64, ambayo Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la chini yake, The Championship, huanzia kampeni zao na nyingine hufuzu toka Raundi zake za awali kabisa.
    Exeter City, Timu ya Ligi 2, ambayo ni Daraja la 4 kwa Mfumo wa England, wamefanikiwa kutinga Raundi ya 3 na sasa ni Wenyeji wa Klabu kigogo Liverpool.

    Raundi hii ya 3 imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe na moja ya hizo ni ile Mechi tamu huko White Hart Lane ambako Tottenham watawavaa ‘Maajabu’ ya Ligi Kuu England Leicester City ambao wako Nafasi ya Pili katika Msimamo wa Ligi hiyo. Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, Jumamosi watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumapili wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
    Siku ya Jumamosi Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.

    FA CUP
    Raundi ya 3
    Ijumaa Januari 8

    22:55 Exeter v Liverpool

    Jumamosi Januari 9
    15:45 Wycombe v Aston Villa
    [Mechi kuanza Saa 12:00 Jioni]
    Arsenal v Sunderland
    Birmingham v Bournemouth
    Brentford v Walsall
    Bury v Bradford
    Colchester v Charlton

    Doncaster v Stoke
    Eastleigh v Bolton
    Everton v Dag & Red
    Hartlepool v Derby
    Huddersfield v Reading
    Hull v Brighton
    Ipswich v Portsmouth
    Leeds v Rotherham
    Middlesbrough v Burnley
    Newport v Blackburn
    Northampton v MK Dons
    Norwich v Man City
    Nottm Forest v QPR
    Peterborough v Preston
    Sheff Wednesday v Fulham
    Southampton v Crystal Palace
    Watford v Newcastle
    West Brom v Bristol City
    West Ham v Wolves
    20:30 Man United v Sheffield United

    Jumapili Januari 10
    15:00 Oxford United v Swansea
    17:00 Carlisle v Yeovil
    17:00 Chelsea v Scunthorpe
    19:00 Tottenham v Leicester
    21:00 Cardiff v Shrewsbury



    THE EMIRATES FA CUP 2015/16
    TAREHE MUHIMU
    Raundi ya 3
    Ijumaa 9 Januari 2016
    Raundi ya 4

    Jumamosi 30 Januari 2016
    Raundi ya 5
    Jumamosi 20 Februari 2016

    Raundi ya 6-Robo Fainali

    Jumamosi 12 Machi 2016

    Nusu Fainali
    Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
    Fainali Jumamosi 21 Mei 2016


    0 maoni:

    Chapisha Maoni