.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Ijumaa, 8 Januari 2016

Tagged Under:

MWANASOKA BORA RAIA WA TANZANIA MBWANA ALLY SAMATTA ANACHEZEA TP MAZEMBE YA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

By: Unknown On: Ijumaa, Januari 08, 2016
  • Share The Gag

  • Mwanasoka raia wa Tanzania   anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.
    Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani.
    Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
    Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
    Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon
    Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo.
    Klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo
    Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon
    Mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Gassama kutoka nchini Gambia
    Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni