.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 13 Februari 2017

Tagged Under:

ANTONIO CONTE AMJIBU JOSE MOURINHO KIMYAKIMYA! 'SIPENDI MZAHA WA MOURINHO!"

By: Unknown On: Jumatatu, Februari 13, 2017
  • Share The Gag

  • Antonio Conte amesema hapendi 'mzaha'wa Jose Mourinho baada ya Meneja huyo wa Manchester United kudai Chelsea ambao ni Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, hawawezi kukamatika kileleni kwa sababu ni Timu 'inayojihami mno!'.
    Hivi sasa Chelsea wapo Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham baada Jana kutoka 1-1 na Burnley huko Turf Moor.
    Mourinho, ambae anasifika kwa kuchota akili za Mameneja wapinzani na kuwavuruga, Juzi alidai Chelsea haiwezi kuteleza kutoka kileleni kwa vile 'wanajihami mno' na kushinda kwa kutumia 'kaunta ataki'.
    Jana Meneja wa Chelsea Antonio Conte alijibu mapigo kwa kusema: "Hiyo ni hadaa yake. Nina uzoefu kuelewa hilo!"
    Mara nyingi Mourinho amekuwa akikwaruzana na Mameneja wenzake kutokana na vijembe vyake vya kuwapandisha munkari ili kushinda vita ya kisaikolojia na muhanga mkuu wa mashambulizi hayo huko nyuma akiwa Arsene Wenger wa Arsenal.

    Hata hivyo Conte amegoma kuburutwa kwenye vita hiyo na kujibu: "Sipendi kujibu kuhusu Makocha wengine!" 

    EPL – Ligi Kuu England
    RATIBA:
    Jumatatu Februari 13

    2300 Bournemouth v Manchester City
    Jumamosi Februari 25
    1800 Chelsea v Swansea City
    1800 Crystal Palace v Middlesbrough
    1800 Everton v Sunderland
    1800 Hull City v Burnley
    Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]
    1800 West Bromwich Albion v Bournemouth
    2030 Watford v West Ham United
    Jumapili Februari 26
    1630 Tottenham Hotspur v Stoke City
    Manchester City v Manchester United[IMEAHIRISHWA]
    Jumatatu Februari 27
    2300 Leicester City v Liverpool
    Jumamosi Machi 4
    1530 Manchester United v Bournemouth
    1800 Leicester City v Hull City
    1800 Stoke City v Middlesbrough
    1800 Swansea City v Burnley
    1800 Watford v Southampton
    1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace
    2030 Liverpool v Arsenal
    Jumapili Machi 5
    1630 Tottenham Hotspur v Everton
    1900 Sunderland v Manchester City
    Jumatatu Machi 6
    2300 West Ham United v Chelsea

    0 maoni:

    Chapisha Maoni