.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatano, 17 Septemba 2014

Tagged Under:

MAMBO 5 MUHIMU DANNY WELBECK KU ‘SHAINI’ ARSENAL

By: Unknown On: Jumatano, Septemba 17, 2014
  • Share The Gag

  • Na Simon Chimbo
    Moja kati ya habari kubwa sana za usajili wa kiangazi msimu huu nchini Uingereza ni uhamisho wa mshambuliaji mwenye nguvu na mbio Danny Welbeck kutoka Manchester United kwenda Arsenal kwa ada ya paundi 16m. kijana huyu mwenye miaka 23 pamoja na kubezwa na mashabiki wengi lakini ana kitu ambacho kwa macho ya kawaida hakikuonekana pale Old Trafford. Ndio maana sivishangai vilio vya wakongwe wa Manchester United kama Paul Scholes, David Becham na Rio Ferdinand wakionesha kusikitishwa kwao kwa kuondoka kwa kijana huyo aliyekulia mjini Manchester tangu akiwa mdogo.
    Zifuatazo ni sababu zinazoweza kumng’arisha Dany Welbeck Arsenal;
    1.Kutaka kuthibitisha uwezo wake
    Welbeck kama ambavyo mchezaji yeyote angeweza fanya, atajituma uwanjani ili kuonesha Manchester United walimuuza kimakosa huku pia akitaka kuwaondoa shaka mashabiki wa Arsenal kwamba mzee Wenger hakukosea kumsajili.
    2. Uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza
    Kuumia kwa Olivier Giroud kunamfanya Dany awe na upinzani mdogo na mshambuliaji aliye fiti Yaya Sanogo. Tofauti na ilivyokua Manchester United, Wayne Rooney na Robin Van Persie walimpa wakati mgumu Welbeck kupata nafasi kikosi cha kwanza huku usajili wa Radamel Falcao ungemfanya asipate nafasi kabisa.
    3. Viungo wa Arsenal
    Tofauti na Manchester United ambapo hakukua na viungo wenye uwezo wa kucheza na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao kufunga magoli, lakini uwezo wa viungo wazuri kama Jack Wilshere, Mesut Ozil, Aaron Ramsey, Carzola na wengine, sina shaka Dany atafunga magoli mengi tofauti na alivyokua Old Trafford.
    4. Matarajio hafifu ya mashabiki wa Arsenal kwa kijana huyo
    Presha sio kubwa kwa Welbeck kufanya vizuri kwa washika mitutu hao wa London kutokana na ukweli kwamba mashabiki wengi wa gunners hawana uhakika na uwezo wa mshambuliaji huyo raia wa Uingereza na hivyo Dany anaweza kucheza vizuri kwani mashabiki hawamtarajii makubwa.
    5.Uwezo wa mwalimu Arsene Wenger

    Wengi mtakubaliana na mimi jinsi Arsene Wenger alivyo wabadilisha wachezaji wake wengi kutoka kua wachezaji wa kawaida hadi kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia kama Aaron Ramsey na wenzake huku akiwa na uwezo mkubwa wa kuwa saikoloji wachezaji wake.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni