.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 5 Januari 2015

Tagged Under:

FA CUP: DROO YA RAUNDI YA 4 KUFANYIKA LEO USIKU. ARSENAL KUCHEZA NA NANI RAUNDI YA 4? CHELSEA, MAN UNITED, MAN CITY?

By: Unknown On: Jumatatu, Januari 05, 2015
  • Share The Gag

  • DROO ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP itafanyika Leo Usiku kabla ya Mechi ya Raundi ya 3 kati ya AFC Wimbledon na Liverpool.
    Miongoni mwa Timu ambazo zitakuwepo kwenye Kapu la Droo hiyo ni Timu ndogo, Sheffield United na Rochdale ambazo zilizibwaga Timu za Madaraja ya juu yao.
    Sheffield United, Timu ya Daraja la Ligi 1, waliitandika Timu ya Ligi Kuu England QPR Bao 3-0 wakati Rochdale, pia Timu ya Daraja la Ligi 1, waliwabwaga Nottingham Forest ambao wamewahi kutwaa FA CUP mara 2.
    Pia kwenye Droo hiyo wapo Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, pamoja na Vigogo wa Ligi Kuu England Chelsea, Manchester United na Manchester City.
    Watakaofanya Droo hiyo ni Mfungaji wa Bao la Wimbledon kwenye Fainali ya FA CUP ya Mwaka 1988, Lawrie Sanchez, akisaidiwa na Stef Loucaides ambae ni Kocha wa Timu ya Wanawake ya U-18 ya Kingstonian.


    TAREHE ZA RAUNDI:
    -Raundi ya 3: 3 Januari 2015
    -Raundi ya 4: 24 Januari 2015
    -Raundi ya 5: 14 Februari 2015
    -Raundi ya 6: 7 Machi 2015
    -Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015
    Fainali: 30 Mei 2015

    0 maoni:

    Chapisha Maoni