.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 27 Aprili 2017

MANCHESTER CITY 0 vs 0 MANCHESTER UNITED, FELLAINI AONESHWA KADI NYEKUND WAKIUMALIZA BILA UBABE ETIHAD U

By: Unknown On: Alhamisi, Aprili 27, 2017
  • Share The Gag

  • Maruane Fellaini ameondeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa City Kun Aguero huku akiwa na kadi ya njano kipindi cha pili. Pia mchezo huo uliomalizika bila ya kufungana kwa kutoka 0-0 umekuwa ni afueni kwa Man United kwa kuendeleza mechi nyingi bila kufungwa msimu huu. Na huku wakionekana kupanda kujihakikishia kuwa kwenye nafasi ya kugombea nafasi ya nne bora ili kucheza Klabu Bingwa msimu ujao. Man City v Man Utd, EPL MANCHESTER DERBY LIVE scoreVIKOSI: 
    MAN CITY: Bravo, Zabaleta, Kompany (C), Otamendi, Kolarov, Fernandinho, Yaya Toure, Sterling, De Bruyne, Sane, Aguero
    Akiba:
    Caballero, Sagna, Fernando, Navas, Clichy, Gabriel Jesus, A. Garcia

    MAN UNITED: De Gea, Valencia, Blind, Bailly, Darmian, Carrick, Herrera, Fellaini, Mkhitaryan, Martial, Rashford.
    Akiba: Romero, Shaw, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Young, Lingard, Rooney



    Jumapili, 23 Aprili 2017

    Kipigo cha Barcelona kwa Real Madrid kilichovunja rekodi ya Real Madrid

    By: Unknown On: Jumapili, Aprili 23, 2017
  • Share The Gag

  • Baada ya kuondolewa katika michuano ya UEFA Champions League kwa timu ya FC Barcelona usiku wa April 23 2017 walisafiri hadi katika jiji la Madrid kuendeleza harakati zao za kuwania Kombe la LaLiga kwa kucheza dhidi ya wapinzania wao wa jadi Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
    Mastaa wa zamani wa Real Madrid Ronaldo de Lima na Luis Figo walikuwepo uwanjani kuangalia game.
    FC Barcelona walisafiri kuelekea Madrid tayari wakiwa wanamkosa mchezaji wao wa kimataifa wa Brazil Neymar kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, licha ya kumkosa Neymar safu ya ushambuliaji ya Barcelona bado ilikuwa imara na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-2.
    Lionel Messi akifunga goli lake la 500 akiitumikia FC Barcelona
    Lionel Messi ndio ameonekana kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22 katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea Lionel Messi faulo dakika ya 77, Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 33 na 90 baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.

    Wakati magoli ya Real Madrid yalifungwa na Casemiro dakika ya 28 na James Rodriguez dakika ya 85 akitokea benchi, ushindi huo wa FC Barcelona unavunja rekodi yaa Real Madrid ambao walikuwa wamecheza mechi 22 bila kufungwa katika uwanja Santiago Bernabeu toka February 27 2016.
    Barcelona anaongoza baada ya ushindi wa leo kwa tofauti ya magoli lakini amemzidi mchezo mmoja Real Madrid

    Alhamisi, 6 Aprili 2017

    MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND 2016/2017 ULIVYO KWA SASA BAADA YA CHELSEA KUIPIGA CITY BAO 2-1.

    By: Unknown On: Alhamisi, Aprili 06, 2017
  • Share The Gag


  • Premier League
    PosLogo &TeamPWDLGDPts
    1ChelseaChelsea3023343872
    2Tottenham HotspurTottenham Hotspur3019833865
    3LiverpoolLiverpool3117952760
    4Manchester CityManchester City3017762358
    5ArsenalArsenal2916672554
    6Manchester UnitedManchester United29141231954
    7EvertonEverton3114981951
    8West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion3112811-144
    9SouthamptonSouthampton2910712-137
    10WatfordWatford3010713-1237
    11Leicester CityLeicester City3010614-1036
    12Stoke CityStoke City319913-1236
    13BournemouthBournemouth319814-1235
    14BurnleyBurnley3110516-1235
    15West Ham UnitedWest Ham United319616-1633
    16Crystal PalaceCrystal Palace309417-1131
    17Hull CityHull City318617-2930
    18Swansea CitySwansea City318419-2928
    19MiddlesbroughMiddlesbrough3041115-1523
    20SunderlandSunderland305520-2920

    Jumanne, 4 Aprili 2017

    JUMATANO EPL NI STAMFORD BRIDGE CHELSEA vs MAN CITY, MANCHESTER UNITED vs EVERTON

    By: Unknown On: Jumanne, Aprili 04, 2017
  • Share The Gag

  • EPL RATIBA
    Jumanne Aprili 4

    2145 Burnley v Stoke City
    2145 Leicester City v Sunderland
    2145 Watford v West Bromwich Albion
    2200 Manchester United v Everton


    MANCHESTER UNITED Jumanne Usiku wako kwao Old Trafford kucheza na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo hiyo na ile inayufuatia Wikiendi inayokuja dhidi ya Sunderland ndiyo itatoa mwelekeo wa Timu hiyo kuwemo 4 Bora au la kwa mujibu wa Meneja wao Jose Mourinho.

    Akiongelea kuelekea Mechi hii na Everton, Mourinho alisema atashusha Kikosi kikali dhidi ya Everton na Sunderland na matokeo ya Mechi hizo ndio yataamua nini hatima yao kwenye Ligi na kwani baada ya hapo watacheza Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI na mkazo utakuwa huko.
    Kufuzu 4 Bora ya Ligi kutawawezesha Man United kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao lakini pia kutwaa EUROPA LIGI kutawapa nafasi hiyo pia.

    Hivi sasa kwenye EPL Man United wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 28 wakati Man City wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 58 kwa Mechi 29.
    Uso kwa Uso
    -Man United hawajafungwa katika Mechi 4 zilizopita na Everton.
    -Katika Mechi 49 za EPL, Man United Ushindi 33 Sare 8 Everton Ushindi 8
    Man United wataingia Mechi hii wakitoka Sare ya 0-0 na West Bromwich wakati Everton walichapwa 3-1 na Liverpool Mechi zote zikichezwa Juzi Jumamosi.
    Sare hiyo kwa Man United imeendeleza wimbi lao la Mechi 19 kutofungwa kwenye Ligi.

    Hali za Vikosi:
    Man United inategemewa kuwa nao tena Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera baada ya kumaliza Vifungo vyao vya Mechi 3 na 2 lakini itawakosa Majeruhi Juan Mata, Chris Smalling na Phil Jones huku pia kukiwepo uwezekano wa Paul Pogba kucheza baada ya kupona maumivu yake na kuanza mazoezi.
    Everton inakabiliwa na Majeruhi 6 wakiwemo Seamus Coleman, alievunjwa Mguu akiichezea Nchi yake Republic of Ireland dhidi ya Wales Wiki ilyopita na pia Sentahafu wao wa Argentina Ramiro Funes Mori alieumia vibaya Goti.

    Pia Mchezaji wa zamani wa Man United Kiungo Morgan Schneiderlin na Winga Aaron Lennon watakosekana kwa kuwa na maumivu.

    Mechi ya Kwanza Msimu huu
    Mapema Mwezi Desemba Zlatan Ibrahimovic aliifungia Bao Man United na Everton kusawazisha Dakika za lala salama kwa Penalti tata iliyotolewa kwa Rafu iliyofanywa na Mchezaji wa zamani wa Everton Marouane Fellaini na Adhabu hiyo kufungwa na Leighton Baines na kuifanya Gemu iishe 1-1.