TANGU
wafungwe 4-0 na Chelsea huko Stamford Bridge hapo Oktoba 23, Manchester
United imekuwa Timu pekee ‘Isiyofungika’ kwenye EPL, Ligi Kuu England,
ikimaliza zaidi ya Miezi 5 bila kufungwa zikiwa ni mbio za Mechi 18. Licha kusakamwa na Mechi kedekede wakiwa Timu pekee wenye Mechi nyingi kupita yeyote huko England, Jose Mourinho ameongoza Kikosi hicho kwa ufanisi mkubwa na kuwawezesha Mwezi Februari kutwa Taji kubwa walipobeba Kombe la Ligi, EFL CUP.
Mwezi Aprili wanakabiliwa na Mechi 9 na ingawa Mourinho amelalamikia ugumu wa Ratiba yao lakini hilo ni dalili tosha ya mafanikio yao Msimu huu wao wa kwanza chini ya Jose Mourinho ambao walikuwemo kwenye mbio za Mashindano Manne na kutolewa tu Wiki 2 zilizopita kwenye FA CUP.
Hilo limempa Mourinho nafasi ya kubadili Kikosi chake katika kila Mashindano na kumwezesha kupata Kikosi imara cha kucheza EPL bila kufungwa.
Mtizame
Mchezaji wa Kimataifa wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, ambae kwenye
Mechi yake ya kwanza tu Klabuni hapo, walipofungwa na Man City Mwezi
Septemba, alitolewa nje lakini hilo halikumkatisha tamaa kwani aliibukia
kwenye UEFA EUROPA LIGI na kung’ara na kurudi tena Kikosi cha Kwanza. Kushiriki Mashindano mengi kumemfanya Mourinho azungushe Wachezaji kwenye kila Mechi ya EUROPA LIGI, EFL CUP na FA CUP lakini kwenye Ligi panga pangua wapo David de Gea; Antonio Valencia, Phil Jones, Marcos Rojo, Matteo Damian; Ander Herrera, Michael Carrick; Henrikh Mkhitaryan/Juan Mata, Paul Pogba, Marcus Rashford; Zlatan Ibrahimovic.
Wafutiliaji wa hizo Mechi zao 18 ambazo hawakufungwa kwenye Ligi wamebaini Man United hufungwa Goli chache, 11 tu, lakini pia kufunga chache, Bao 29 tu.
Hiyo ndiyo sababu kubwa Man United wako Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa Pointi 17 nyuma ya Vinara Chelsea.
Kwa ujumla Man United wamefunga Bao 42 katika Mechi 27 za Ligi tofauti na wenzao kama Liverpool waliofunga 62, Chelsea 59, Tottenham Hotspur 55, City 54, Arsenal 56 na Everton 51.
Kitu muhimu kwa Kikosi cha Mourinho kutofungwa Mechi 18 za Ligi ni Difensi yake hasa ule upacha wa Sentahafu ya Marcos Rojo na Phil Jones huku Ander Herrera akiwa nguzo kubwa kwenye Kiungo.
Walipofungwa Mechi yao ya mwisho ya Ligi na Chelsea, upacha wa Sentahafu ulikuwa ni wa Eric Bailly na Chris Smalling na kuumia kwao kukatoa mwanya kwa Rojo-Jones kucheza pamoja na wao ni kati ya Wachezaji 6 waliocheza Mechi nyingi kwenye hizo 18 ambazo hawakufungwa wakifuatia Herrera, Ibrahimovic, Pogba na Kipa De Gea anaeongoza.
Lakini tatizo kubwa ni ufungaji ambao umebaki kwa Zlatan Ibrahimovic pekee aliefunga Jumla ya Mabao 26 Msimu huu na 11 kati ya Mechi 16 za Ligi zilizopita.
Sasa Mwezi Aprili Man United wanakabiliwa na Mechi 9 wakianzia Jumamosi Old Trafford kucheza na West Brom na kisha Jumanne Everton watatua Uwanja huo huo wakati Jumamosi inayofuatia watakuwa safarini Stadium of Light kuivaa Timu ya Mkiani Sunderland inayoongozwa na Meneja wa zamani wa Man United David Moyes.
Mbio hizi za kutofungwa za Mechi 18 za Ligi ndio bora kabisa kwenye Ligi Kuu England tangu Machi 2013 pale Kikosi chini ya Sir Alex Ferguson kilivyofanya hivyo.





Ferguson amekuwa Meneja wa United kwa miaka 27 kwenye miaka ya 1986 na 2013
Juan Mata(kushoto) akipongezwa na wenzake kwa bao lake la pekee katika mchezo huo wa marudiano.
cha
pili dakika ya 70 Juan Mata aliwafungia Man United bao na kubadilisha
matokeo ya awali na kuwa (2-1 kwenye Agg.) Hku katika Mchezo huo wa
raundi ya 16 Man United wakimbadilisha Paul Pogba dakika ya 48 aliyeumia
na kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Fellaini. Manchester United
pia walimbadilisha Beki Blind dakika ya 64 na kumuingiza Jones. Pia
katika mchezo huo Zlatan alicheza vyema kipindi cha kwanza na kidogo
afunge aligonga mwamba.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Man Unied 0 Rostov 0.


Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15
(Serengeti Boys) katika siku yake ya kwanza nchini katika kuadhimisha
miaka 100 ya benki ya standard Chartered tangu kuanzishwa kwake.
Afisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ujio wa John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya
miaka 15.
Timu
ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho
baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya
Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth
Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja
na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata
nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.