Tagged Under:
UCHAGUZI WA RAIS FIFA KUENDELEA LICHA MAAFISA 7 KUBAMBWA KWA RUSHWA!
By:
Unknown
On: Alhamisi, Mei 28, 2015
FIFA
imesema Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho hilo utaendelea Ijumaa licha ya
Maafisa wao 7 kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi
ya Dola 150 Milioni.
Ijumaa Kongresi ya FIFA inapiga Kura za
Uchaguzi wa Rais ambapo Rais wa sasa, Sepp Blatter, anawania kiti hicho
kwa mara ya 5 huku akikabiliwa na Mpinzani mmoja, Mwana wa Mfalme Ali
bin al-Hussein kutoka Jordan.
Maafisa waliobambwa Leo kwa tuhuma za
rushwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb, na Eduardo Li,
Julio Rocha, Costas Takkas, Eugenio Figueredo, Rafael Esquivel na Jose
Maria Marin.
Maafisa
wa Polisi wa Uswisi waliivamia Hoteli ya Baur au Lac Mjini Zurich
ambayo Wajumbe wa FIFA wamefikia kwa ajili ya Uchaguzi wa Ijumaa na
kuwanasa Maafisa hao 7 kutokana na Mashitaka yaliyofunguliwa na Idara ya
Sheria ya Marekani ambayo imefungua Mashitaka 47 kwa Watuhumiwa 14
wanaodaiwa kuhusika na rushwa na utakatishaji Fedha kwa kipindi cha
Miaka 24.
Hata hivyo, Rais wa FIFA, Sepp Blatter, hajahusishwa na Mashitaka hayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni