Tagged Under:
CAF YAIPA TANZANIA UENYEJI FAINALI ZA U17, SHUKRAN KWA RAIS KIKWETE!
By:
Unknown
On: Jumatano, Mei 27, 2015
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji
wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka
2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza
soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali
hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi
Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya
vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya
wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF
inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na
inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha
mashindano haya mwaka 2019.
0 maoni:
Chapisha Maoni