2-3(Ag
2-4) ndivyo majibu yalivyokuwa mpaka dakika ya mwisho ya dakika ya 90
na Barca kuibuka na Ushindi huku mchezaji wao matata Neymar akiifungia
bao 2.
Neymar
aliwafungia bao la tatu Barcelona baada ya kuwachomoka mabeki wa
Atletico Madrid kwa kuwakacha na Jordi Alba kutoa pasi aliyoimalizia
Langoni Neymar katika dakika ya 41.
Bao
la kusawazisha Barca wamejifunga wenyewe Atletico Madrid kupitia kwa
Miranda katika dakika ya 38 baada ya kumalizia mpira uliopigwa kona.
Dakika ya 30 Raúl García aliifungia bao la pili Atlletico Madrid na
kufanya 2-1 kwa mkwaju wa penati. Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Nou
Camp Wiki iliyopita, Barcelona waliibuka washindi kwa Bao 1-0 kwa Bao
la Dakika ya 85 la Lionel Messi ambalo alilifunga baada ya Penati yake
kuokolewa na Kipa na Mpira kumrudia tena na kuukwamisha wavuni na hivyo
Barcelona kusonga Nusu Fainali kwa Jumla ya Mabao 4-2 na watakutana na
Mshindi kati Getafe na Villareal ambao katika Mechi yao ya kwanza,
Villareal alishinda Bao 1-0.
Kwenye Mechi ya usiku huu, Fernando Torres aliipa Atletico Bao la kuongoza na Neymar kusawazisha.
Kisha
Penati ya Raul Garcia ikawapa Atletico Bao la Pili lakini Beki wao
Miranda akajifunga mwenyewe na Neymar akaipa Barca Bao la 3 na la
ushindi.
Balaa kwa Atletico lilikuja pale Gabi alipopewa Kadi
Nyekundu wakati wa Haftaimu Wachezaji wakielekea Vyumba vya Kubadili
Jezi na Mario Suarez kufuatia mwishoni.
Dakika ya 9 Neymar aliwasawazishia bao barcelona na kufanya 1-1 (Agg
ikiwa 1-2). Bao hilo lilipatikana baada ya Luis Suarez kutoa pande kwa
Neymar.

Dakika
ya 1 tu Fernando Torres anaichapa bao Barca na kufanya 1-0 dhidi ya
Timu ya Barcelona baada ya kupata mpira kutoka kwa Guilherme Siqueira.

1-0 Torres aliweka bao la kwanza mapeeema ndani ya dakika 1

Mechi ya Kwnza Messi aliifungia bao Baca
VIKOSI:
ATLETICO MADRD XI (4-4-1-1): Oblak; Juanfran, Miranda, Gimenez, Siqueira; Gabi, M Suarez, Raul Garcia; Ardia, Griezmann, Torres
AKIBA: Moya, Gamez, Lucas, Saul, Cani, Jimenez, Mandzukic
BARCELONA XI (4-3-3): Stegen; Pique, Mascherano, Alba, Alves; Busquets, Iniesta, Rakitic; L Suarez, Messi, Neymar
AKIBA: Masip, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Adriano, Mathieu
