Ushindi huu wa Blatter umekuja baada ya kugubikwa na Kashfa ya Rushwa iliyotokana na hatua ya Marekani kufungua Mashitaka kwa Maafisa wa FIFA kwa tuhuma za rushwa Siku moja tu kabla Uchaguzi huo kufanyika.
Ingawa katika Raundi ya Kwanza ya Kura si Blatter wala Mpinzani wake Prince Ali bin Al Hussein alieshinda Theluthi mbili ya Kura ili kushinda Uchaguzi huo wa Uraisi baada ya Blatter kupata Kura 133 na Prince Ali kupata 73, kitu ambacho kingepeleka Kura kupigwa tena, Mjordan huyo aliamua kubwaga manyanga na kukubali kushindwa.


0 maoni:
Chapisha Maoni