Tagged Under:
COPA AMERICA: ARGENTINA YASONGA HATUA YA NUSU FAINALI BAADA YA KUIFUNGA COLOMBIA KWA MIKWAJU YA PENATI 5-4
By:
Unknown
On: Jumamosi, Juni 27, 2015
Argentina
wameingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, COPA
AMERICA, baada ya kuitoa Colombia kwa Mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia
Sare ya 0-0 katika Dakika 90 kwenye Mechi ya Robo Fainali iliyochezwa
Alfajiri hii.
Katika piga nikupige ya Penati, Timu zote zilifunga
Penati zao 3 za kwanza kupitia Lionel Messi, Ezequiel Garay na Ever
Banega kwa Argentina huku Colombia wakifunga kupitia James Rodriguez,
Radamel Falcao na Juan Cuadrado.
Kwenye Penati ya 4, Muriel akakosa kwa Colombia na Lavezzi kuifungia Argentina na kufanya ngoma iwe 4-3.
Colombia
wakafunga Penati yao ya 5 kupitia Cardona na Argentina, wakitakiwa
kufunga Penati yao ya 5 ili wasonge, wakakosa Mpigaji akiwa Lucas Biglia
na kufanya Bao ziwe 4-4.
Ndipo
zikaja nyongeza za Penati moja moja kuamua Mshindi wa papo kwa papo na
Colombia kukosa Mpigaji akiwa Zuniga lakini Argentina nao wakakosa
ushindi baada ya Marcos Rojo kukosa pia.
Penati iliyofuatia ilipigwa
na Colombia lakini Murillo akakosa na akaja Mchezaji mpya wa Boca
Juniors ya Argentina, Carlos Tevez, alieanzia Benchi kwenye Mechi hii,
na kufunga Penati ya mwisho iliyowapa Argentina ushindi wa Penati 5-4.
0 maoni:
Chapisha Maoni