Mara nyingi nimesikia ndani ya vikao vya
Bunge kuhusu ishu ya jinsi kuwahamisha watu wanaoishi pembeni ya
Viwanja vya ndege ili Viwanja vitanuliwe.. kuna waliofuata Viwanja na
kuanzisha makazi yao, ishu ni Kiwanja kiondoke kwenda mbali au watu
waondolewe viwanja vitanuliwe?
Nimekutana na hii ripoti ya Daily Mail iliyotolewa June 04 2015.. inaonesha Viwanja vya Ndege vilivyojengwa mbali zaidi na Miji.

Oslo-Torp Airport..
Huu uwanja uko umbali wa Kilometa 117 kutoka Oslo ambapo ni Mji Mkuu wa
Norway. Ukitaka kufika Town inabidi utumie taxi au usafiri wa treni.

Munich West Airport.
Ukisikia jina la huu Uwanja unaweza kuhisi kwamba uko ndani ya Mji Mkuu
wa Ujerumani, Munich. Lakini ukweli ni kwamba Uwanja huu wa ndege
uko Memmingen. Na bado Umbali wa kutoka Uwanjani mpaka kwenye Mji ni
Kilometa 112.

Frankfurt (Hahn). Uwanja huu wa Ndege uko umbali wa kama kilometa 109 kutoka Mji wa Frankfurt, Ujerumani.
0 maoni:
Chapisha Maoni