.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Alhamisi, 2 Aprili 2015

Tagged Under:

RATIBA: BUNDESLIGA HII JUMAMOSI, BORUSSIA DORTMUND vs BAYERN MUNICH... HAPATOSHI!!

By: Unknown On: Alhamisi, Aprili 02, 2015
  • Share The Gag

  • Jumamosi Signal Iduna Park itakuwa na kivumbi kikubwa wakati Wenyeji Borussia Dortmund watakapocheza na Mahasimu wao wakubwa wa Miaka ya hivi karibuni Mabingwa Bayern Munich.
    Licha ya kuwa Msimu huu Bayern wanaelekea kuutwaa Ubingwa kilaini wakiwa Pointi 10 mbele kileleni na Dortmund kujikwamua toka mkiani na sasa wako Nafasi ya 10, Mechi hii Siku zote haikosi ushindani.
    Hivi karibuni ushindani huu umeongezeka kwa uhasama baada ya Bayern 'kuwapora' Dortmund Mastaa wao Robert Lewandowski na Mario Goetze.
    Pengine hali hiyo, ikichanganywa na kukumbwa na Majeruhi kibao, ndio ilisababisha Dortmund kupwelepweta Msimu huu.
    Hali hii sasa imewageukia Bayern ambao wana Majeruhi wa Mastaa wao wakubwa, Arjen Robben, ambae ndie Mfungaji wao bora, na David Alaba huku Franck Ribbery akiwa na hatihati kucheza kutokana na maumivu.
    www.bukobasports.comBUNDESLIGA
    RATIBA
    Jumamosi Aprili 4

    16:30 Bayer Levkn v Hamburger SV
    16:30 Eintracht Frankfurt v Hannover 96
    16:30 Sport-Club Freiburg v 1. FC Köln
    16:30 SV Werder Bremen v 1. FSV Mainz 05
    16:30 TSG 1899 Hoffenheim v Borussia Mönchengladbach
    16:40 VfL Wolfsburg v VfB Stuttgart
    19:30 Borussia Dortmund v Bayern Munich

    Jumapili Aprili 5
    16:30 FC Augsburg v Schake
    18:30 Hertha BSC v SC Paderborn 07

    0 maoni:

    Chapisha Maoni