
Mwezi Januari, Wenger, ambae ni Meneja wa Arsenal, aliiponda Tuzo hiyo ya FIFA anaetunukiwa Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka na kusisitiza kuwa angepewa nafasi ya kupiga Kura asingekubali.

Cristiano Ronaldo, ambae aliwahi kucheza chini ya Mourinho alipokuwa Real Madrid, ndie anaeshikilia Tuzo hiyo kwa sasa baada ya kuitwaa kwa mara ya 3 Mwezi Januari.

Mourinho alisema: "Nadhani Wenger alisema kitu cha maana, anapinga Ballon d’Or, na nadhani yuko sahihi kwa sababu kwa sasa Soka linapoteza mvuto wa Kitimu na kutilia mkazo Mtu binafsi!"
Mourinho alinena: "Sasa tunatizama ubinafsi. Fulani na takwimu zake kwamba alikimbia umbali mrefu. Kwa sababu kwenye Gemu umekimbia Kilomita 11 na mie nimekimbia 9 wewe ndio umefanya kazi nzuri? Pengine siyo! Labda Kilomita zangu 9 ni muhimu kuliko zako 11! Kwangu mie Soka ni Kitimu. Mtu binafsi anakaribishwa ikiwa anataka kufanya Timu yetu iwe bora!''

0 maoni:
Chapisha Maoni