Chelsea
na Paris Saint-Germain zimetoka 1-1 katika Mechi ya Kirafiki ya
michuano ya International Champions Cup huko Bank of America Stadium,
North Carolina lakini Chelsea wamepata ushindi baada kupigiana Penati
kwa kupata Penati 6-5.
Majuzi, Chelsea walitwangwa Bao 4-2 katika Mechi yao ya kwanza na New York Red Bulls.
Bao
za mechi hii zilifungwa na Zlatan Ibrahimovic, Dakika ya 25, kwa PSG na
lile la Chelsea kufungwa na Victor Moses katika Dakika ya 65.
Kwenye Mikwaju ya Penati, KIpa wa Chelsea, Thibaut Courtois, aliokoa Penati mbili.
Zikiwa
zimebki Dakika 25, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimuingiza Straika
wao mpya alietoka kwa Mkopo kutoka AS Monaco, Radamel Falcao.
Kipa wa Chelsea akiachia na kumfunga kipa mwenzake wa PSG

Akiokoa mkwaju wa Penati

Radamel Falcao akipigana vikumbo kuutafuta mpira dhidi ya Marquinhosvies

Kipa wa Chelsea Thibaut akiokoa jahazi langoni mwake

Thiago Motta na John Terry

Blaise Matuidi na Nemanja Matic

Wachezaji wa PSG wakimpongeza mwenzao Zlatan baada ya kufunga bao kipindi cha kwanza
0 maoni:
Chapisha Maoni